Unyama!Masten Wanjala,20,Akiri Kuteka Nyara, Kunyonga Watoto Wawili Kabete

Muhtasari
  • Masten Wanjala,20,Akiri Kuteka Nyara, Kunyonga Watoto Wawili Kabete
Mshukiwa Masten Milimu Wanjala
Image: DCI

Masten Milimu Wanjala, kijana wa miaka 20 amekiri kuteka nyara, kunyonga watoto wawili  huko Kabete.

Wanjala alikamatwa hapo awali na maafisa wa upelelezi kutoka kwa DCI katika eneo la Shauri Moyo kwa tuhuma za kuua watoto wawili wenye umri wa miaka 13 na 12 kwa tarehe tofauti.

Watoto hao, waliotambuliwa kama Charles Opindo Bala, 13 aliyepotea mnamo Juni 30, 2021, na Mutuku Musyoka, 12 ambaye alipotea Julai 8, walipatikana kwenye kichaka huko Kabete, Kaunti ya Kiambu.

Katika ufichuzi mpya, Wanjala amekiri kuwateka nyara na kuwanyonga watoto hao.

Aliongoza maafisa wa upelelezi mahali ambapo alifanya vitendo vya kinyama na kuitoa miili hiyo huko Kabete.

Kabla ya hapo, Wanjala alikuwa amewasiliana na mama wa Musyoki, Felista Wayua, akidai fidia ya Shilingi 50,000 ili mtoto wake awe huru.

Baba ya Opindo Tony Opindo, ambaye mtoto wake hakuwahi kurudi nyumbani kutoka Shule ya Msingi Sagaret huko Majengo, aliulizwa kutuma Shilingi 30,000 kununua uhuru wa mtoto wake.