Rais Kenyatta alaani vikali mauaji mwanamazingira mashuhuri Kiambu

Joanna anakumbukwa sana kwa juhudi zake katika kulinda msitu wa Kiambu dhidi ya kuvamiwa na watu

Muhtasari

•Kupitia ujumbe uliotolewa na ikulu asubuhi ya Ijumaa, kiongozi wa taifa ametambua juhudi za mwanadada huyo katika kutunza mazingira nchini Kenya.

•Kenyatta aliagiza wapelelezi kuchunguza waliotekeleza unyama huo kwa dharura.

Image: HISANI

Rais Uhuru Kenyatta ameatibu vikali mauaji ya mwanamazingira Joanna Stuchburry

Kupitia ujumbe uliotolewa na ikulu asubuhi ya Ijumaa, kiongozi wa taifa ametambua juhudi za mwanadada huyo katika kutunza mazingira nchini Kenya.

Kenyatta aliagiza wapelelezi kuchunguza waliotekeleza unyama huo kwa dharura.

"Ni jambo la kusikitisha sana kuwa watu waovu wamekatiza maisha ya Joanna Stuchburry kinyama . Jonna amekuwa bingwa katika kutuza mazingira na anakumbukwa sana kwa juhudi zake kulinda msitu wa Kiambu dhidi ya kuingiwa na watu" Rais alisema.

Stuchburry alipigwa risasi nne na kuuliwa siku ya Alhamisi  akiwa nyumbani  maeneo ya Kiambu.

Rais Kenyatta aliombea familia ya marehemu iweze kupata nguvu ya kustahimili msiba huo.