Covid-19:Watu 11 waaga dunia,769 wapona,503 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa vipya 503 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4.060 chini ya saa 24 zilizopita
  • Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 194,310  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 12.4%
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 472 ni wakenya ilhali 31 ni raia wa kigeni,251 ni wanaume huku 252 wakiwa wanawake
Virusi vya Korona
Virusi vya Korona
Image: Hisani

Kenya imesajili visa vipya 503 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4.060 chini ya saa 24 zilizopita.

Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 194,310  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 12.4%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 472 ni wakenya ilhali 31 ni raia wa kigeni,251 ni wanaume huku 252 wakiwa wanawake.

Kulingana na wizara ya afya watu 11 wameaga dunia kutokana na viruis vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 3,811 ya walioaga dunia.

Jumla ya wagonjwa 769 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 183,980, 523 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 246 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,253 ambao wamelazwa hospitalini,3,966 wamejitenga nyumbani.

Pia kuna wagonjwa 140 kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 1,636,475