Wizara ya elimu nchini imetangaza kupunguzwa kwa karo ya shule katika shule za upili.
Hii ni kutokana na ufupi wa kalenda ya masomo ya mwaka wa 2021.
Wanafunzi katika shule za kitaifa kwa saa watalipa Shilingi 45,054 baada ya karo ya awali kupunguzwa kwa shilingi 8500.
Karo ya shule za kaunti na zingine imepunguzwa kwa shilingi 5500 na kufikia 39,554.
Mwaka mpya wa masomo unatarajiwa kuanza wiki ijayo baada ya wanafunzi kupatiwa likizo ya wiki moja tu mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mengi yatafuata...