Covid-19: Watu 1,006 wapatikana na corona,13 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 1,006 wamepatikana maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 5,584 ambazo zilipimwa ndani ya 24
  • Kati ya maambukizi hayo mapya mgonjwa wa umri wa chini ana wiki 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Watu 1,006 wamepatikana maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 5,584 ambazo zilipimwa ndani ya 24.

Kati ya maambukizi hayo mapya mgonjwa wa umri wa chini ana wiki 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93.

Vile vile wagonjwa 485 ni wanaume ilhali 521 ni wanawake, pia 966 ni raia wa kenya huku 40 wakiwa ni raia wa kigeni.

Jumla ya visa vya maambukizi ya corona nchini imefika 199,941 kutoka kwa jumla sampuli 2,109,581.

Aidha watu 261 wamepona maradhi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 187,824 ya watu waliopana corona,33 wamepona huku wakipokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 228 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoa hospitali tofauti nchini.

Kuna wagonjwa 1,386 waliolazwa hospitalini ilhali wagonjwa 3,686 wamejitenga nyumbani.

Wagonjwa 174 wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Pia watu 13 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 3,895ya watu walioangamia kutokana na corona.