(+Picha) Hafla ya mazishi ya afisa Caroline Kangogo aliyeripotiwa kujitoa uhai yaendelea

Mwili wa Caroline ulivalishwa gauni la harusi kama alivyokuwa ameomba kupitia ujumbe wa simu.

Muhtasari

•Hafla ya mazishi  ya afisa Caroline Kangogo aliyeripotiwa kujiotoa uhai mnamo Julai  16 iling'oa nanga asubuhi ya Alamisi.

•Mamia ya waombolezaji ikiwemo maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Nakuru alikokuwa anahudumu Bi Caroline walihudhuria. 

Jeneza la marehemu Caroline Kangogo
Jeneza la marehemu Caroline Kangogo
Image: MATHEWS NDANYI

Hafla ya mazishi  ya afisa Caroline Kangogo aliyeripotiwa kujiotoa uhai mnamo Julai  16 iling'oa nanga asubuhi ya Alamisi.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwa gari la kubebea maiti na maafisa wa polisi hawakuhusishwa kwenye shughuli hiyo.

Wazazi wa Caroline, Bw Barnabas Kangogo na Bi Leah Kangogo waliongoza waombolezaji kuchukua mwili wa  marehemu kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Iten.

Wazazi wa marehemu Caroline Kangogo, Bwana Barnabas Kangogo na Bi Leah Kangogo
Wazazi wa marehemu Caroline Kangogo, Bwana Barnabas Kangogo na Bi Leah Kangogo
Image: MATHEWS NDAYI

Mwili wa Caroline ulivalishwa gauni la harusi kama alivyokuwa ameomba kupitia ujumbe wa simu.

Kakake marehemu, Mark Kangogo alisema kuwa dadake  alikuwa mtu mzuri licha ya yale yaliandikwa kumhusu kwenye vyombo vya habari. Alisema kuwa familia itamfanyia marehemu mazishi ya heshima.

Mamia ya waombolezaji ikiwemo maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Nakuru alikokuwa anahudumu Bi Caroline walihudhuria. 

Aliyekuwa bwana wa Caroline, Bw. Ngeno pia alihudhuria hafla hiyo.