logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Covid-19: Watu 346 wapatikana na corona, 1,404 wapona

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,367,077.

image
na Radio Jambo

Habari30 August 2021 - 12:07

Muhtasari


  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 333 ni wakenya ilhali 13 ni raia wa kigeni,161  ni wanaume huku 185 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 235,298 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 9.7%
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa 346 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 3,553 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 333 ni wakenya ilhali 13 ni raia wa kigeni,161  ni wanaume huku 185 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 235,298 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 9.7%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,367,077.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 3, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 10 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,720 ya walioaga dunia.

Vile vile watu 1,404 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 222,357.,  1,327 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 77 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa  1,951 ambao wamelazwa hospitalini, 5,924 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 148 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,752,266

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved