logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ulinzi wa Ruto, Savula ataka baadhi ya polisi kuondolewa

Savula alisema kuwa si vyema kwa polisi wanaofaa kuwapa wakenya ulinzi watumike kulinda mali ya mtu binafsi.

image
na Radio Jambo

Burudani03 September 2021 - 05:26

Muhtasari


• Savula alisema kuwa si vyema kwa polisi wanaofaa kuwapa wakenya ulinzi watumike kulinda mali ya mtu binafsi.

Mbunge wa Lugari Ayub Savula

Mbunge wa Lugari Ayub Savula amesema kuwa walinzi ambao wanalinda mali binafsi ya Naibu wa Rais William Ruto wanafaa kuondolewa.

Savula ambaye alikuwa akizungumzia suala la ulinzi wa naibu rais ambaye wandani wake walikuwa wamedai kwamba amepokonywa walinzi.

Waziri wa usalama Fred Matyang'i hata hivyo alipuuzilia mbali madai hayo akisema kwamba naibu rais ana ulinzi wa kutosha akiwa amepewa jumla ya maafisa 257 wa polisi huku baadhi yao wakitumika kulinda mali yake ya kibinafsi.

Savula alisema kwamba polisi hao wanafaa kurejeshwa kwenye vituo vyao ili wachangie kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao kwani utakuwa ni uchaguzi wa mpito na utahitaji usalama wa hali ya juu.

Savula alikuwa akizungumza siku ya Alhamis katika kanisa la P.A.G Bahati wakati wa Ibaada ya wafu ya aliyekuwa mwanachama wa ANC Macleans Sloya.

Alisema kuwa si vyema kwa polisi wanaofaa kuwapa wakenya ulinzi waendeleze shughuli za kulinda mali ya mtu binafsi.

Tayari waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i aliweka bayana orodha ya polisi wanaolinda mali mbali mbali za naibu rais suala ambalo limezidi kuibua mjadala mkali nchini.

Savula pia alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wakenya kwamba kinara wa ANC Musalia Mudavadi atakuwa kwa debe la urais mwaka 2022.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved