logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi waagizwa kuondoa vizuizi barabarani

Polisi waagizwa kuondoa vizuizi barabarani

image
na Radio Jambo

Burudani07 September 2021 - 08:35

Muhtasari


• Vile vile, hakuna gari linalopaswa kuzuiliwa barabarani kwa muda mrefu bila maelezo.

• Makamanda polisi katika kaunti kuhakikisha kuna usimamizi wa karibu oparesheni za trafiki.

Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai

Maafisa wa polisi kwa mara nyingine tena wameonywa dhidi ya kuweka vizuizi vyovyote vya barabarani mahali popote bila idhini rasmi.

Vile vile, hakuna gari linalopaswa kuzuiliwa barabarani kwa muda mrefu bila maelezo.

Maagizo haya yaliafikiwa katika mkutano kati ya Inspekta Jenerali wa polisi Hilary Mutyambai naibu wake Edward Mbugua, makamanda wa mkoa na makamanda wa kaunti jijini Nairobi.

Mawasiliano kutoka Mbugua yalisema mkutano huo ulibaini kuwa kuna baadhi ya maafisa watovu wa polisi ambao bado wanaweka vizuizi vya barabarani bila idhini licha ya mwongozo wa hapo awali.

"Leo asubuhi, nimeelekeza kwamba kituo kidogo cha Trafiki cha Ainabkoi kiondolewe kwa kuendelea kuweka kizuizi barabarani, kuzuliwa magari kwa muda mrefu bila sababu na malalamiko kuhusu kuitisha rushwa kutoka kwa waendesha magari licha ya maagizo ya awali yaliyotolewa kwa usimamizi wa Trafiki," alisema Mbugua katika ujumbe wake kwa makamanda wa kaunti tarehe 3 Septemba.

Alimwambia kila kamanda kuhakikisha kuwa hakuna vizuizi vya barabarani, ukaguzi wa trafiki katika eneo moja, hakuna kuzuia agari kando ya barabara kwa muda mrefu na hakuna kuchukua rushwa kutoka kwa waendeshaji magari ndani ya mamlaka yao.

Aliwaambia makamanda kuhakikisha kuna usimamizi wa karibu oparesheni za trafiki.

Alisema ikiwa malalamiko yatatolewa na umma kuhusu ukiukaji wa maagizo hayo, uchunguzi utafanywa ili kuepusha udhalilishaji.

"Hata hivyo ikiwa ukweli utabainika kwa kukiuka maagizo hatua kali zinachukuliwa dhidi ya afisa atakayekuwa amehusika.

Aliwaambia makamanda kuhakikisha kuna usimamizi wa karibu oparesheni za trafiki.

"Nitaitisha mkutano wiki ijayo kuunda mkakati mzuri na kukagua hatua tukazokuwa tumeafia juu ya mada hii," alisema.

Hii ni mara ya tatu kwa mwaka kwamba makamanda wa polisi wanakutana kujadili suala la usimamizi wa trafiki.

Mkutano huo ulifanyika katika Banda la Polisi jijini Nairobi mnamo Septemba 2.

Agizo la awli lilisema kuwa kizuizi chochote cha barabara kilichoidhinishwa lazima kiwe na maafisa kutoka idara mbali mbali na sio kwa sababu za mtu binafsi kujitajirisha.

Hii ilifuata malalamiko ya umma kwamba vizuizi bado vinawekwa licha ya agizo la mapema la kuziondoa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved