Covid-19:Watu 649 wapatikana na corona,30 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 649 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,704 chini ya saa 24 zilizopita
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Watu 649 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,704 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 639 ni wakenya ilhali 10 ni raia wa kigeni,295 ni wanaume huku 354 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 241,783 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.4%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,429,337.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 4, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 116.

Hata hivyo watu 30 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,830 ya walioaga dunia.

Aidha watu 333 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 230,095, 221 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 112 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,790 ambao wamelazwa hospitalini, 4,419 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 162  katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).