Majambazi wamuua kinyama mlinzi Busia

Muhtasari

• Awali genge hilo lilijaribu kuvunja nyumba yake katika eneo la Obekai bila mafanikio.

 

crime scene
crime scene

NA LEONARD ACHARRY 

Majambazi waliokuwa wamejihi kwa panga na shoka wamemuua mlinzi wa baa moja katika soko la Tangakona kaunti ndogo ya Nambale kaunti ya Busia na kuiba mali ya thamani isiojulikana usiku wa kuamkia Alhamisi.

Mwenye baa hiyo Charles Kaunda Atelu  alisema wezi hao ambao idadi yao haikujulikani walimpiga na kumuua mlinzi huyo mwendo wa saa nane usiku kabla ya kuiba pombe, na vifaa vya burudani ukiwemo mtambo wa jenereta.

Awali genge hilo lilijaribu kuvunja nyumba yake katika eneo la Obekai bila mafanikio.

Wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Amukura ya kati Moses Ouma waliwaomba maafisa wa polisi kuzidisha juhudi za kuwakamata majambazi hao ambao wameendeleza visa vya wizi na mauaji katika maeneo mbali mbali ya kaunti ndogo ya Nambale katika siku za hivi majuzi.