logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto ataka shamba ‘lake la Laikipia’ kupewa wafugaji

Ruto ataka shamba ‘lake la Laikipia’ kupewa wafugaji

image
na Radio Jambo

Burudani09 September 2021 - 12:45

Muhtasari


• Ruto ambaye alizungumza kwa majazi alisema ameipa serikali idhini kuchukuwa shamba hilo ili kuwapa wananchi wenye mifungo kutumia kama malisho yao

Naibu rais Wiliam Ruto sasa anataka shamba ambalo waziri Fred Matiang’i alisema ni lake katika eneo la Laikipia ligawiwe wananchi wa eneo hilo.

Ruto ambaye alizungumza kwa majazi alisema ameipa serikali idhini kuchukuwa shamba hilo ili kuwapa wananchi wenye mifungo kutumia kama malisho yao kwa lengo la kudhibiti utovu wa usalama katika eneo hilo.

“Mimi nataka niwambiye Wale walisema ya kwamba ati mimi niko na shamba kule Laikipia ekari 15,000, mimi nataka niwaambiye kwa sababu nyinyi mumesema hiyo shamba iko, na ni yangu sasa mimi nawapatia authority, hiyo shamba ekari 15,000 mnayosema ni yangu endeni mgawanye mpatiye wananchi”, Ruto alisema.

Wiki iliyopita waziri wa usalama wa ndani Fred Matyang’i akiwa mbele ya kamati ya bunge kujibu maswali kuhusu ulinzi wa naibu rais alisema kwamba naibu rais alikuwa anamiliki mashamba mbali mbali nchini ikiwemo ekari kadhaa katika eneo la Laikipia.

Naibu rais hata hivyo alijibu madai ya Matyangi alikanusha baadhi ya mali iliyotajwa akisema kwamba ni asilimia 70 pekee ya mali zilizotajwa na Matyangi zilizokuwa zinamilikiwa naye.

Ruto hata hivyo siku ya Alhamisi akizungumzia utovu wa usalama katika eneo la Laikipia hali ambayo imepelekea baadhi ya wakazi kupoteza maisha, wengine kujeruhiwa na mamia kutoroka makwao Ruto alitaka shamba hilo lipewe wenyeji ‘kama lipo’.

“Eeh… si wamesema mimi niko na shamba huko sasa mimi nimesema kwa sababu nyinyi mko na details, sasa muwagawanyie wananchi wa Laikipia ndiyo waweze kulisha ng’ombe wao”, naibu rais alisema.

Naibu rais alimkashifu inspekta mkuu wa polisi kuhusu utendakazi wake na kumtaka kuachana na mambo ya siasa na badala yake kuangazia usalama wa wananchi.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved