Makali ya corona: Watu 661 wapatikana na corona,533 wapona ,32 waaga dunia

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 640 ni wakenya ilhali 21 ni raia wa kigeni,332 ni wanaume huku 329 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 2412,945 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.1%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Watu 661 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 8,141 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 640 ni wakenya ilhali 21 ni raia wa kigeni,332 ni wanaume huku 329 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 2412,945 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.1%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,444,357.

Mgonjwa wa umri wa chini ana siku 11, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 102.

Hata hivyo watu 32 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,896 ya walioaga dunia.

Aidha watu 533 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 230,940, 416 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 117 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,723 ambao wamelazwa hospitalini, 4,725 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 174  katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).