Maaskofu wa Katoliki wapiga marufuku hotuba za wanasiasa kanisani

Muhtasari

•Maaskofu hao wamesema kwamba mwanasiasa yeyote ambaye anahudhuria misa wanafaa kufanya vile kama waumini wengine bila kutarajiwa huduma maalum.

Archbishop Antony Muheria
Archbishop Antony Muheria
Image: EUTYCAS MUCHIR

Maaskofu wa kanisa la Katoliki wamepiga marufuku hotuba za wanasiasa kanisani wakati wa ibada ya  misa.

Maaskofu hao wamesema kwamba mwanasiasa yeyote atakayehudhuria misa anafaa kufanya vile kama waumini wengine bila kutarajiwa huduma maalum.

Wamesema kwamba hakuna mwanasiasa atakubaliwa kujipigia debe kanisani ama kuhutubia waumini katika maeneo ya ibada.

Maaskofu hao wamesema kuwa vuta nikuvute iliyo kati ya rais na naibu wake William Ruto ni hatari kwa amani na utulivu wa nchi.

"Tunahofia kwamba iwapo mzozo huo utachukuliwa na wafuasi basi athari amabyo unaweza kuleta nchini utakuwa ngumu kutafakari" Maaskofu hao wamesema.

Archbishop Antony Muheria
Archbishop Antony Muheria
Image: EUTYCAS MUCHIR