Makali ya corona:Kenya imesajili visa 446 vipya vya maambukizi ya corona

Muhtasari
  • Watu 446 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,406 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 435 ni wakenya ilhali 11 ni raia wa kigeni,227 ni wanaume huku 2019 wakiwa wanawake
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS

Watu 446 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,406 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 435 ni wakenya ilhali 11 ni raia wa kigeni,227 ni wanaume huku 2019 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 244,826 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 7.0%.

Mgonjwa wa umri wa chini ana wiki 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,470,865.

Hata hivyo watu 21 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,949 ya walioaga dunia.

Aidha watu 459 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 235,196, 331 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 128 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,525 ambao wamelazwa hospitalini, 3,341 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 118  katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).