Nnamdi Kanu aishtaki Kenya kwa kumrudisha nyumbani

Muhtasari

• Kundi lake la Indigenous People of Biafra (Ipob), ambalo linataka kujitenga kwa jimbo la kusini -mashariki mwa Nigeria limetambuliwa na serikali kama kundi la kigaidi.

Nnamdi Kanu, akionekana kuwa kuzuizini alikamatwa kutoka mwezi Juni
Nnamdi Kanu, akionekana kuwa kuzuizini alikamatwa kutoka mwezi Juni
Image: Nigeria Presidency

Kiongozi wa kundi linalotaka kujitenga nchini Nigeria Nnamdi Kanu, amewashtaki maafisa wa Kenya kwa kile anachosema ni kufurushwa kiharamu kwenda Nigeria.

Kundi lake la Indigenous People of Biafra (Ipob), ambalo linataka kujitenga kwa jimbo la kusini -mashariki mwa Nigeria limetambuliwa na serikali kama kundi la kigaidi.

Bw. Kanu, ambaye kwa sasa yuko kizuizini, alizuiliwa nchini Nigeria mwezi Juni baada yakusafirishwa nchini humo, lakini mamlaka hazikutoa ufafanuzi kuhusu mahali alipokamatwa.

Familia yake awali ilisema alikamatwa nchini Kenya, lakini mamlaka za Kenya hazijathibitisha madai hayo.

Nyaraka za mahakama zilizonukuliwa na vyombo vya Habari nchini Kenya, zinadai kuwa kuzuiliwa kwake kulienda kinyume na sheria ya Kenya ya kumuondoa mtu nchini humo na hali kadhalika kikatiba.

“Mhusika anaaminiwa kukamatwa katika uwanja wa ndege mnamo Juni 19, 2021 na kuzuiliwa kwa siku kadhaa na baadaye kusafirishwa kiharamu nchini Nigeria bila pasipoti yake ya Uingereza bila kuzingatia muongozo wa sheria za,” ombi lililonukuliwa katika gazeti la Punch linasema.