Shule za kitaifa kusalia chini ya mtaala wa CBC

Muhtasari

• Shule za upili zitahifadhi hadhi zao za kitaifa, shule maalum za kaunti na kaunti ndogo chini ya mtaala mpya.

NA LEWIS NYAUNDI 

Shule za upili zitahifadhi hadhi zao za kitaifa, shule maalum za kaunti na kaunti ndogo chini ya mtaala mpya.

Hata hivyo, mfumo utakaotumiwa na wizara ya Elimu kuwaweka wanafunzi wa CBC kwa shule ya upili bado haijabainika.

Walakini, uthibitisho kwamba shule zitabaki na hadhi yao umesababisha wasiwasi kwani wanafunzi wengi kutoka shule za msingi huenda watapendelea kujiunga na shule kuambatana na hadhi zao.

Mwenyekiti wa muungano wa wazazi nchini Kenya Nicholas Maiyo anasema Hatua hii huenda ikaibua mgogoro mkubwa miongoni mwa wanafunzi wanapong’ang’ania nafasi katia shule za kitaifa  ii italeta wasiwasi juu ya uwezekano wa kurudi kwa ushindani mkali, ili kupata nafasi katika shule za kitaifa chini ya mtaala mpya.

Katibu wa kuhudumu wa Utekelezaji wa Mageuzi ya Mitaala katika wizara ya Elimu, Fatuma Chege hata hivyo alipepezea chini hofu hii akibainisha kuwa kugawanywa kwa shule hakuhusiani na matokeo ya wanafunzi.

Chege alisema lengo ni kuhakikisha kuwa watoto watajiunga na shule zilizo na vifaa vya kutosha kuhakikisha wanatimiza mahitaji yao ya elimu katika shule ya upili.

 “Hadhi shule za kitaifa, kaunti ya ziada, kaunti, kaunti ndogo haitafafanua ubora wa elimu, ni kile kinachotokea ndani ya shule na ndani ya nafasi ya darasa.

“Lebo hiyo haitafanya muujiza wowote, ni kile kinachotokea darasani, kinachotokea katika mazingira ya shule.

“Lazima tuweke mwelekeo wetu katika kile kinachoendelea ndani ya darasa na ndani ya shule. Hiyo ndiyo itakayomtoa mtoto katika mfumo wowote ulimwenguni,” Chege alisema.

Afisa mkuu mtendaji mkuu wa Baraza la Mitihani la Kenya David Njegere aliunga mkono hoja akibainisha kuwa kusudi la tathmini ya malezi sio kuwaorodhesha watoto.

"Sio kusema ni mtoto gani bora kuliko yule mwingine, ni kutafuta tu wapi kila mtoto na ni uingiliaji gani tunahitaji kuweka ili kuhakikisha watoto wanaweza kupata," Njegere alisema.