Bei ya petroli: wabunge na maseneta wanafaa kuwajibika

Muhtasari

• Lita moja ya mafuta ya petroli mjini Nairobi sasa inauzwa kwa shilingi 134 huku takriban asilimia 60 ya bei hiyo ikiwa ni kodi unaotozwa na serikali.

Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli
Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli
Image: MAKTABA

Wabunge na maseneta wametakiwa kuajibikia maslahi ya wakenya na kusaidia katika kudhibiti bei za bidhaa muhimu nchini.

Gavana wa kakamega Wycliffe oparanya siku ya Alhamisi aliwataka wabunge na maseneta kuwajibika na kushughulikia kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini.

Oparanya ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa mipango ya serikali alisema kwamba nyongeza ya bei ya mafuta imeathiri pakubwa maisha ya wananchi wa kawaida amabo walikuwa tayari wanakabiliwa na changamoto cha kiuchumu kutokana na athari za janga la Corona.

Oparanya
Oparanya

Taasisi za kifedha na masuala ya kiuchumi tayari zimeonya kuhusu mfumko wa bei za bidhaa kutokana na kuongezaka marudufu kwa bei za mafuta nchini.

Lita moja ya mafuta ya petroli mjini Nairobi sasa inauzwa kwa shilingi 134 huku takriban asilimia 60 ya bei hiyo ikiwa ni kodi unaotozwa na serikali.