Ndugu wawili wapiga ndugu yao mkubwa hadi kifo kwa kushambulia mama yao juu ya chakula Busia

Muhtasari

•Kulingana na DCI, marehemu alikuwa ametoka kupiga maji usiku wa Jumatano na kuagiza chakula kutoka kwa mama yake ila akafahamishwa kwamba hakikuwa tayari.

•Juma hakupendezwa na jibu hilo na hapo akaanza kumshambulia mamake kwa ngumi na mateke kwani alidhani alikuwa ananyimwa chakula.

•Ambao walifika kumuokoa ni wanawe wengine wawili Odhiambo na Ouma ambao walipiga ndugu yao mkubwa kwa ngumi, mateke na silaha za aina tofauti kisha wakaenda kulala.

crime scene 1
crime scene 1

Polisi wanazuilia ndugu wawili ambao wanadaiwa kushambulia ndugu yao mkubwa na kumuacha katika hali mahututi.

Juma 32, alifariki kutokana na majeraha mabaya mwilini ambayo aliugua kufuatia kichapo kikubwa  alichopokea kutoka kwa ndugu zake Pascaliano Odhiambo 29 na Bonventure Ouma 19 nyumbani kwao katika eneo la Butula, kaunti ya Busia..

Kulingana na DCI, marehemu alikuwa ametoka kupiga maji usiku wa Jumatano na kuagiza chakula kutoka kwa mama yake ila akafahamishwa kwamba hakikuwa tayari.

Juma hakupendezwa na jibu hilo na hapo akaanza kumshambulia mamake kwa ngumi na mateke kwani alidhani alikuwa ananyimwa chakula.

Mwanamke huyo alianza kupiga mayowe makubwa akiomba kunusuriwa kutoka mikononi mwa mwanawe ambaye hakuwa na huruma yoyote kwake.

Ambao walifika kumuokoa ni wanawe wengine wawili Odhiambo na Ouma ambao walipiga ndugu yao mkubwa kwa ngumi, mateke na silaha za aina tofauti kisha wakaenda kulala.

Asubuhi ya kuamkia Alhamisi mama yao alipoenda kumjulia hali mwanawe aliyekuwa amepigwa vibaya alipatwa na mshtuko kumuona akiwa amelala nje ya mlango wa chumba chake akiwa na jeraha kubwa kichwani.

Hapo akapiga ripoti kwa maafisa wa usalama ambao walituma wapelelezi kutoka Butula wakachunguze kilichokuwa kimetokea.

Upanga mkali, jembe na rungu  ambazo zinaaminika kutumika kuangamiza marehemu zilipatikana kwenye eneo la tukio na zinahifashiwa kama ushahidi katika kituo cha polisi.

Ndugu wawili ambao walihusika kwenye shambulio hilo walikamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka.