Makali ya corona: Watu 404 wapatikana na corona,231 wapona

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 390 ni wakenya ilhali 14 ni raia wa kigeni,206 ni wanaume huku 198 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 249,174 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.4 %
Waziri wa afya Mutahi Kagwe
Image: Twitter

Kenya imesajili visa 404 vipya vya maambukizi ya Covid-19 siku ya JUmapili kutoka kwa sampuni 6,309 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 390 ni wakenya ilhali 14 ni raia wa kigeni,206 ni wanaume huku 198 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 249,174 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.4 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,549,996.

Hata hivyo watu 3 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,119 ya walioaga dunia.

Aidha watu 231 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 241,411 159 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 72 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,042 ambao wamelazwa hospitalini, 2,247 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 75 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

JUmla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,712,030.