Covid-19:Jumla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika watu 3,761,876 na 260 wamepatikana na corona

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 249,434 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.2 %
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,556,222
Image: HISANI

Kenya imesajili visa 260 vipya vya maambukizi ya Covid-19 siku ya JUmapili kutoka kwa sampuni 6,226 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 256 ni wakenya ilhali 4 ni raia wa kigeni,140 ni wanaume huku 120 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 249,434 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.2 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,556,222.

Hata hivyo watu 4wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,123 ya walioaga dunia.

Aidha watu 109 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 241,520 ,78 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 31 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,021 ambao wamelazwa hospitalini, 2,193 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 66 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

JUmla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,761,876.