Mkewe Isaac Mwaura akabiliana na msongo wa mawazo

Muhtasari

• Mukami alisema siku zingine hata kupata nguvu za kuamka asubuhi na kufanya kazi huwa changamoto.

Mke wa Isaac Mwaura Nelius Mukami Picha: KWA HISANI
Mke wa Isaac Mwaura Nelius Mukami Picha: KWA HISANI

Nelius Mukami, mke wa mwanasiasa Isaac Mwaura, anasema kwamba msongo wa mawazo ndicho kitu cha gharama zaidi anachomiliki.

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, Mukami alisema kuishi na msongo wa mawazo, wasiwasi na kuhisi kupuuzwa (ADHD) ni moja ya mambo magumu ambayo amelazimika kupitia maishani.

"Imechukua mengi kutoka kwangu na inaendelea kuchukua. Inachukua juhudi nyingi kuizuia na bado inaniathiri hata katika siku zangu za furaha na wakato nikiwa mpweke."

Mukami alisema siku zingine hata kupata nguvu za kuamka asubuhi na kufanya kazi huwa changamoto.

"Hakuna anayeelewa kuwa inachukua kila kitu ndani yangu kujivuta kutoka kitandani," alisema.

"Msongo wa mawazo unaendelea kunipotezea mambo ambayo nimeyaona, kumbukumbu na watu. Ninajikuta nikisononeka na kutostahili.

"Nimepoteza sehemu zangu nyingi sana, wakati mwingine mimi hujitazama kwenye kioo na siwezi kujitambua mimi ni nani tena."

Katika mahojiano ya awali na Word Is, Mukami alisema amekuwa katika hali mbaya tangu kupoteza watoto wake wawili kati ya mapacha watatu aliokuwa amepata.

"Nimekuwa nikipambana na msongo wa mawazo tangu mwaka 2018 mwezi Aprili, mara tu baada ya kutoka hospitalini," alisema.

"Safari yangu ya afya ya akili imekuwa mzunguko mkubwa na ngumu sana kuelezea kwa sababu sio wengi wataelewa.

"Watu wanadhani ni hali ya akili tu ambayo unaweza tu kuiondoa kwa kujipa motisha ya kutosha lakini sio ... Angalau sio kwangu."

Alisema anashukuru kwa kila siku kuwa anaishi.

"Ninajua chini kabisa kwamba sijapromoka na ninathamani. Najua bado kuna mengi kwangu kushinda.