Polisi wachunguza moto katika CBK Kisumu

Muhtasari

• Kiwango cha uharibifu, uliotokana na moto huo katika eneo hilo lenye ulinzi mkali bado hakijabainika.

crime scene
crime scene

Polisi wanachunguza kisa cha moto kilichotokea katika Benki Kuu ya Kenya mjini Kisumu.

Sababu ya moto huo wa Alhamisi usiku ambao ulizuka karibu saa tano usiku ilikuwa bado haijafahamika.

Maafisa wa polisi katika kituo cha karibu cha Polisi cha CBK walikimbilia eneo la tukio na kuanza kuzima moto kabla ya zimamota wa kaunti ya Kisumu kuwasili.

Kiwango cha uharibifu, uliotokana na moto huo katika eneo hilo lenye ulinzi mkali bado hakijabainika.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kisumu Richard N'geno alisema ni kisanduku cha udadilishanaji kilichoharibika.

"Moto ulitoka kwenye sanduku la kubadili maji kwenye bango la barabara," Ng'eno alisema.

Alisema kikosi cha wachunguzi kilikuwa tayari kimeundwa ili kuchunguza tukio hilo na kubaini chanzo cha moto.

"Hakuna kitu kingine chochote kilichoharibiwa mbali na kisanduku cha kubadili. Sababu ya moto haijafahamika lakini uchunguzi umeanza," Ngeno alisema.

Tukio hilo limetokea wiki tatu baada ya tukio lingine la moto kuteketeza ofisi za idara ya mipango katika Jumba la Prosperity mjini Kisumu.