Makali ya corona: Watu 308 wapona corona,91 wapatikana na corona,9 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 250,114 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.7 %
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,572,609
  • Hata hivyo watu 9 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,140 ya walioaga dunia
Image: HISANI

Kenya imesajili visa 91 vipya vya maambukizi ya Covid-19 siku ya Ijumaa kutoka kwa sampuni 3,435 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 88 ni wakenya ilhali 3 ni raia wa kigeni,50 ni wanaume huku 41 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 250,114 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.7 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,572,609.

Hata hivyo watu 9 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,140 ya walioaga dunia.

Aidha watu 308 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 242,535,241 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 67 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 918 ambao wamelazwa hospitalini, 1,944 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 56 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

JUmla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,874,083.