Jamaa kutoka Siaya aua mwenzake aliyemkejeli kuwa mkewe alikuwa kiruka-njia kabla amuoe

Muhtasari

•Inadaiwa kwamba Marvin aliambia George kwamba alikuwa anasaidiwa na wanaume wengine kutosheleza mkewe na hapo ndipo mshukiwa akapandwa na mori na kutoa fimbo ambayo alitumia kumgonga vibaya kichwani.

crime scene 1
crime scene 1

Jamaaa mmoja kutoka kaunti ya Siaya anawindwa na wapelelezi kwa kuua jirani yake kisha kukimbia mafichoni.

George Onyango (28) anaripotiwa kugonga jirani yake Marvin Onyango (30) kichwani kwa kutumia rungu katika kijiji cha Onyoso, eneo bunge la Gem.

Kulingana na DCI, wawili hao walikuwa wanazozana kabla ya mshukiwa kutoa rungu na kuitumia kuangamiza mwenzake kisha kuenda mafichoni.

Uchunguzi wa awali umebaini kwamba mshukiwa alijawa na ghadhabu baada ya marehemu kumkejeli kuwa alioa mke ambaye alikuwa amelala na wanaume wengi hapo awali.

Inadaiwa kwamba Marvin aliambia George kwamba alikuwa anasaidiwa na wanaume wengine kutosheleza mkewe na hapo ndipo mshukiwa akapandwa na mori na kutoa fimbo ambayo alitumia kumgonga vibaya kichwani.

Wapelelezi wameanza juhudi za kuwinda mshukiwa ili ajibu mashtaka ya mauaji dhidi yake.