logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Afueni kwa Wakenya waliochanjwa Corona, Uingereza kuwaruhusu kusafiri bila kuwekwa kukarantini

Balozi wa Uingereza nchini Kenya Jane Marriot alitangaza kuwa Wakenya waliochanjwa dhidi ya COVID-19 ambao watasafiri kuenda UK kutoka wiki ijayo hawatalazimika kupimwa wala kuenda karantini kabla ya kufunga safari.

image
na Radio Jambo

Habari08 October 2021 - 02:23

Muhtasari


• Balozi wa Uingereza nchini Kenya Jane Marriot alitangaza kuwa Wakenya waliochanjwa dhidi ya COVID-19 ambao watasafiri kuenda UK kutoka wiki ijayo hawatalazimika kupimwa wala kukarantini kabla ya kufunga safari.

•Baada ya kuwasili Uingereza Wakenya  na raia wengine wa kigeni ambao wamechanjwa wanahitajika kupimwa ndani ya kipindi cha siku mbili za kwanza baada ya kuwasili

Kamishna Mkuu wa UK nchini Kenya

Ni faraja kwa Wakenya waliochanjwa dhidi ya Covid-19 na ambao wanapanga kusafiri Uingereza baada ya serikali ya taifa hilo kuwaruhusu kuingia bila kulazimika kukarantini.

Balozi wa Uingereza nchini Kenya Jane Marriot alitangaza kuwa Wakenya waliochanjwa dhidi ya COVID-19 ambao watasafiri kuenda UK kutoka wiki ijayo hawatalazimika kupimwa wala kukarantini kabla ya kufunga safari.

Msemaji wa Kamishna Mkuu wa Uingereza alisema kuwa hatua ya Uingereza kutambua vyeti vya chanjo kutoka Kenya ilifanikishwa kufuatia ushirikiano mzuri na wizara ya afya nchini.

"Tuna raha kutangaza kuwa kutoka Jumatatu Oktoba 11, wale ambao wamepokea chanjo Kenya wataweza kusafiri kuenda UK bila kukarantini ama kupimwa kabla ya safari. Shukran kwa ushirikiano mkubwa na wizara ya afya, tumemaliza hatua ya kutambua vyeti vya chanjo kutoka Kenya" Msemaji huyo alisema.

Marriot alisema kuwa hatua hii ni afueni haswa kwa watalii na wafanyibiashara ambao wamekuwa wakihangaika tangu mwanzo wa janga la Corona.

"Hii ni habari njema kwa watu wetu, biashara na watalii baada ya kipindi kigumu cha miezi 18. Ningependa kushukuru wizara ya afya na waziri Mutahi Kagwe kwa ushirikiano mzuri kufanikisha haya" Alisema Marriot.

Kabla ya safari, Wakenya waliochanjwa kikamilifu ambao wanapanga kuenda Uingereza watahitajika kulipia kipimo cha COVID-19  kitafanywa baada ya kuwasili huko.

Baada ya kuwasili Uingereza Wakenya  na raia wengine wa kigeni ambao wamechanjwa wanahitajika kupimwa ndani ya kipindi cha siku mbili za kwanza baada ya kuwasili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved