Watu 3 wamekufa katika ajali ya barabara Makueni

Muhtasari
  • Watu watatu wamekufa katika ajali mbaya ya barabarani katika Kaunti ya Makueni
Image: George Owiti

Watu watatu wamekufa katika ajali mbaya ya barabarani katika Kaunti ya Makueni.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Makueni Joseph Ole Napeiyan alisema watatu hao walifariki papo hapo baada ya magari mawili ya kibinafsi kugongana ana kwa ana karibu na kambi ya barabara ya China kando ya Barabara ya Tawa - Bumbuni katika kaunti ndogo ya Mbooni Mashariki.

Napaiyen alisema miili hiyo ilipelekwa katika Hospitali ya Tawa Level 4.

Waathiriwa watatu wa ajali wamelazwa katika kituo hicho cha afya.

Image: Geoge Owiti

Mengi yafuata;