Makali ya corona:Kenya imerekodi visa 65 vipya vya maambukizi ya corona

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 65 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 3,198 chini ya saa 24 zilizopita
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,613,052
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: HISANI

Kenya imesajili visa 65 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 3,198 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 61 ni wakenya ilhali 4 ni raia wa kigeni,38 ni wanaume huku 27 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 251,313 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.0%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,613,052.

Vile vile watu 296 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 244,533,279 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 17 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hata hivyo watu 5 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,195 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 712 ambao wamelazwa hospitalini, 1,711 wamejitenga nyumbani.

HUku hayo yakijiri kuna wagonjwa 43 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).