Wanaume 2 wamekamatwa kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa miaka 16 Bomet

Muhtasari
  • Wanaume 2 wamekamatwa kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa miaka 16 Bomet
Pingu
Image: Radio Jambo

Wanaume wawili wa umri wa miaka 19 na 22 wamekamatwa hii leo kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa miaka 16 huko Sotik kaunti ya Bomet.

Linus Nyakundi, 19 na Danface Makori, 22 wanashukiwa kumfungia msichana wa shule huko Sudan Waliokaa ndani ya kituo cha biashara cha Sotik huko Tembwo ambapo wanadaiwa walifanya kitendo hicho.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai George Kinoti, alisema wawili hao walionekana na mkazi anayehusika, ambaye aliripoti kwa mkuu msaidizi wa eneo hilo kuwaona wawili hao mapema wakiwa na msichana mchanga.

"Wanaume wawili wa umri wa miaka 19 na 22 wamekamatwa hii leo kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa miaka 16 huko Sotik kaunti ya Bomet

Wanaume hao wanadaiwa kujifungia na kumnajisi mwanafunzi huyo katika chumba cha kulala katika hoteli moja eneo la Tembwo

Baba yake alimtishia mwathiriwa, endapo ataripoti isa hicho kwa polisi

Hata hivyo, arobaini za mwizi zilifika leo baada ya binti huyo kupasua mbarika kwa mamake, na ripoti hiyo kuandikishwa katika kituo cha polisi cha Kola, huko Kilungu Makueni.

Mtoto huyo amepelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi huku.."DCI Ilisema.

Kulingana na ripoti ya polisi, washukiwa walijisalimisha tu baada ya kuwasili kwa maafisa wa Sotik ambao walimwokoa msichana huyo anayesoma katika shule ya upili ya eneo hilo na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi wa kimatibabu.

Kufuatia kuongezeka kwa visa vya ubakaji na unajisi, DCI imeonya wanaume wanaowinda wanawake.

Mwezi uliopita, washukiwa wawili walikamatwa huko Lamu kwa kosa la kumbaka mwanamke mwenye ulemavu wa akili wakati wakijifanya kuwa Wasamaria wema.