Mahakama kuu yaharamisha Huduma namba

Jaji Jairus Ngaah asema utaratibu wa sheria haukufuatwa katika mchakato wa utoaji wa huduma namba

Muhtasari

•Jaji Jairus Ngaah amesema kuwa serikali haikufuata sheria kabla ya kuanza kusambaza kadi hizo mnamo Novemba 18, 2020.

court
court

Mahakama kuu imefutilia mbali utoaji wa kadi za Huduma namba ikiamuru kuwa hatua hiyo haikuwa halali.

Jaji Jairus Ngaah amesema kuwa serikali haikufuata sheria kabla ya kuanza kutoa kadi hizo mnamo Novemba 18, 2020.

Jaji alisema kuwa serikali ilikosea kwa kukosa kutathmini athari za kadi hizo kwa usalama wa maelezo (data) ya watu binafsi  kabla ya kuzisambaza.

Jaji Ngaah ameagiza serikali kutathmini athari za  hatua hiyo kwa  usalama wa data kabla ya kuazisha  tena hatua ya usambazaji.

Mwaka uliopita taasisi ya Katiba pamoja na wakili Yash Pal Ghai  waliwasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya serikali wa kusambaza kadi za huduma bila kutathmini usalama wa maelezo ya wananchi.