logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Makali ya corona: Watu 156 wapatikana na corona,101 wapona

Kuna wagonjwa 596 ambao wamelazwa hospitalini, 1,582 wamejitenga nyumbani.

image
na Radio Jambo

Habari16 October 2021 - 14:15

Muhtasari


  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 8 huku mwenye umri wa juu akiwa na umri wa miaka 87
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 154 ni wakenya ilhali 2 ni raia wa kigeni,91 ni wanaume huku 65 wakiwa wanawake

Kenya siku ya JUmamosi imesajili visa 156 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,408 chini ya saa 24 zilizopita.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 8 huku mwenye umri wa juu akiwa na umri wa miaka 87

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 154 ni wakenya ilhali 2 ni raia wa kigeni,91 ni wanaume huku 65 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 251,959 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.5%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,635,120.

Vile vile watu 101 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 245,178,71 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 30 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Aidha watu 5 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,215 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 596 ambao wamelazwa hospitalini, 1,582 wamejitenga nyumbani.

HUku hayo yakijiri kuna wagonjwa 31 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved