logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Covid-19:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,691,050

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,743,182.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri09 November 2021 - 13:21

Muhtasari


  • Kuna wagonjwa 403 ambao wamelazwa hospitalini, 1,077 wamejitenga nyumbani
  • Huku hayo yakijiri kuna wagonjwa 30 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
  • Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,691,050

Kenya imesajili visa 26 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 1,346 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 25 ni wakenya huku1 akiwa ni raia wa kigeni,16 ni wanaume huku  10 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 253,879 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.9%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,743,182.

Vile vile watu 88 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,458,83 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 5 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.Watu 2 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadii jumla ya walioaga dunia ikifika 5,314

Kuna wagonjwa 403 ambao wamelazwa hospitalini, 1,077 wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri kuna wagonjwa 30 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,691,050.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved