Covid-19:Kiwango cha maambukizi kimefika asilimia 1.3%,64 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 5 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 94
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,215 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.3%
Image: HISANI

Watu 64  wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,790 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 57 ni wakenya huku 7 wakiwa ni raia wa kigeni,38 ni wanaume huku 26 wakiwa wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 5 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 94.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,215 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.3%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,761,828.

Aidha watu 47 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,574,30 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 17 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Mtu mmoja ameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,316.

Kuna wagonjwa 396 ambao wamelazwa hospitalini, 1,044 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 31 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,93,466.