Raila apangiwa makaribisho ya kufana Nyeri

Muhtasari

• Mlima Kenya umekuwa uwanja mkubwa wa ushindani baina ya Raila na Ruto.

• Ruto amepiga kambi katika eneo hilo tangu Jumamosi, akizunguka vijijini kudumisha ushawishi wake.

• Kabla ya hafla hiyo ya Jumamosi, mabaraza ya wazee ya Wajaluo na Wakikuyu yatafanya mkutano wa kihistoria mjini Nyeri mnamo Novemba 26 ili kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya jamii hizo mbili.

KAREN: Raila Odinga akiwa na wazee wa Kikuyu na wanasiasa nyumbani kwake Karen. Picha: KWA HISANI
KAREN: Raila Odinga akiwa na wazee wa Kikuyu na wanasiasa nyumbani kwake Karen. Picha: KWA HISANI

Washirika wa Rais Uhuru Kenyatta kutoka eneo la mlima Kenya wanaandaa makaribisho ya kufana kwa mkutano mkuu wa kisiasa kuidhinisha azma ya urais ya Raila Odinga ya mwaka 2022 wiki ijayo.

Uidhinishaji huo mnamo Novemba 27 mjini Nyeri utafanyika siku tatu tu kabla ya Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa Jubilee ambapo Naibu Rais William Ruto atafukuzwa rasmi kutoka naibu kiongozi wa chama hicho.

Katika mkutano mkuu wa wajumbe, Rais Kenyatta anatarajiwa kufichua mipango yake ya urithi huku akiidhinisha mkataba wa kabla ya uchaguzi wa 2022 na ODM ya Raila.

Siku tisa baada ya chama cha Jubilee kuandaa mkutano wake wa wajumbe, Raila atatangaza rasmi azma yake ya urais ambayo wadadisi wa mrengo wake wake wanaiita bora zaidi kuwahi kutokea.

Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu, mshirika mkuu wa Rais na mratibu wa Azimio La Umoja ya Kati, alisema hafla ya Nyeri itatetemesha wakosoaji wa Handshake.

"Hii itakuwa siku ambayo eneo la kati litazungumza kwa sauti na wazi kuhusu njia yao ya kisiasa ya 2022," Ngunjiri aliambia Star.

Mlima Kenya umekuwa uwanja mkubwa wa ushindani baina ya Raila na Ruto.

Ruto amepiga kambi katika eneo hilo tangu Jumamosi, akizunguka vijijini kudumisha ushawishi wake.

Maelezo yaliyopatikana kutoka kwa wanasiasa wanaoshughulikia mkutano wa Nyeri yanaonyesha hafla kubwa iliyopangwa kutuma ujumbe mkali wa kisiasa na kusisitiza uungwaji mkono wa wazee wa Kikuyu na Wajaluo.

Kabla ya hafla hiyo ya Jumamosi, mabaraza ya wazee ya Wajaluo na Wakikuyu yatafanya mkutano wa kihistoria mjini Nyeri mnamo Novemba 26 ili kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya jamii hizo mbili.

Kuhusika kwa wazee kutoka pande zote mbili kutakuwa ishara ya tamati ya dhana ya kuwepo kwa uhasama baina ya Wakikuyu na Wajaluo iliyoanzia enzi za hayati rais Jomo Kenyatta na Jaramogi Odinga.

Mnamo Jumatatu, mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kikuyu Wachira Kiago alithibitisha kuwa mabaraza hayo mawili ya wazee yatafanya hafla kubwa katika uwanja wa Kabiruini huko Nyeri kabla ya mkutano wa Raila wa Azimio La Umoja.

Mhariri: Davis Ojiambo