Mwanafunzi wa kidato cha 4 auawa Bungoma

Muhtasari

• Walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanafunzi huyo alikuwa anavuka barabara alipogongwa na pikipiki iliyokuwa imebeba abiria  mmoja  ikitoka eneo la Kimabole kuelekea mjini Cheptais na kufariki alipofikishwa kwenye hospitali

crime scene
crime scene

Mwananafunzi mmoja wa kike mtahiniwa wa kidato cha nne katika shule ya upili ya Friends School  kimabole eneo la Chesikaki katika kaunti ya Bungoma ameaga dunia baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabara katika soko la Melon wadi ya Chesikaki.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanafunzi huyo alikuwa anavuka barabara alipogongwa na pikipiki iliyokuwa imebeba abiria  mmoja  ikitoka eneo la Kimabole kuelekea mjini Cheptais na kufariki alipofikishwa kwenye hospitali.

Abiria aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo alipata majeraha mabaya huku mhudumu huyo wa bodaboda aliyesababisha ajali hiyo akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Chesikaki huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Kwa sasa wakaazi wa soko hilo wametoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu wanapovuka barabara huku wito ukitolewa kwa idara husika kuweka vizuizi vya kudhibiti mwendo wa kasi ili kuzuia ajali kutokea.