COVID 19: Wagonjwa 1339 wanapokea matibabu, Asilimia ya maambukizi ni 1.4%

Muhtasari

•Kufikia sasa watu 3,981,902 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 2, 393, 885 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Corona kwa sasa ni 1.4% huku wizara ya afya ikitangaza visa vipya  59 nchini kutoka kwa sampuli ya watu 4,336 ambao wameweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita.

Kufikia sasa Kenya imewahi kurekodi visa 254, 688 kutoka kwa jumla ya vipimo 2, 794, 810 ambavyo vimewahi kufanywa tangu mwanzo wa janga la Corona.

Kaunti ya Nyamira  imeripoti visa vingi zaidi (14 ) ikifuatwa na Nairobi 11 huku kaunti zingine zikiripoti visa chini ya vitano.

Wagonjwa 45 wameweza kupona, 23 wakiponea nyumbani huku 22 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya. Kufikia sasa watu 247, 919 wamewahi kupona maradhi hayo.

Idadi ya vifo nchini kutokana na COVID 19 bado imesimamia 5, 325 kwani hakuna kifo chochote kutokana na COVID 19 kilichoripotiwa leo.

Kwa sasa wagonjwa 4354 wanahudumiwa hospitalini huku wengine 985 wakipokea matibabu kutoka manyumbani kwao. Wagonjwa 21 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia sasa watu 3,981,902 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 2, 393, 885 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.