COVID 19: Asilimia ya maambukizi ni 0.7%, Vifo 3 vyaripotiwa

Muhtasari

•Wagonjwa 35 wameweza kupata afueni ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita, na kufikisha idadi ya waliowahi kupona nchini hadi 246, 027.

•Kufikia jana watu 3, 986,501 walikuwa wamechajwa kikamilifu huku wengine 2,401,926 wakiwa wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Wizara ya afya hivi leo imeripoti visa vipya 22 vya waathiriwa wa COVID 19 kutoka kwa sampuli ya watu 3, 191 waliopimwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Kiwango cha maambukizi nchini kwa sasa ni 0.7%  huku jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa ikifikia 254, 710.

Kaunti ya Nairobi iliripoti visa vingi zaidi leo (8) ikifuatwa na Bomet (6).

Wagonjwa 35 wameweza kupata afueni ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita, na kufikisha idadi ya waliowahi kupona nchini hadi 246, 027.

Jumla ya walioangamia kutokana na maradhi hayo sasa imefikia 5, 328 baada ya vifo 3 zaidi kuripotiwa.

Kwa sasa wagonjwa 350 wamelazwa hospitalini  huku wengine 981 wakiendelea kuhudumiwa nyumbani. Wagonjwa 20 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia jana watu 3, 986,501 walikuwa wamechajwa kikamilifu huku wengine 2,401,926 wakiwa wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona.

Kufikia sasa serikali ya Kenya imeweza kupeana chanjo 6, 388, 427.