Magavana, mawaziri na makatibu wasusia mkutano wa Ruto

Muhtasari

• Ni magavana tisa pekee, waziri mmoja na makatibu wawili wa kudumu waliofika kwa mkutano muhimu na Naibu Rais William Ruto. 

• Waziri wa Ugatuzi Charles Keter, Naibu Waziri wa Ugatuzi Julius Muia (Hazina) na Julius Korir Julius (Ugatuzi) pekee ndio waliohudhuria mkutano wa BEC ulioongozwa na naibu rais William Ruto.

Naibu Rais William Ruto. Picha: TWITTER/WILLIAM RUTO
Naibu Rais William Ruto. Picha: TWITTER/WILLIAM RUTO

 Ni magavana tisa pekee, waziri mmoja na makatibu wawili wa kudumu waliofika kwa mkutano muhimu na Naibu Rais William Ruto. 

Waziri wa Ugatuzi Charles Keter, Naibu Waziri wa Ugatuzi Julius Muia (Hazina) na Julius Korir Julius (Ugatuzi) pekee ndio waliohudhuria mkutano wa baraza maalum la Bajeti ya Serikali na Uchumi (IBEC) ulioongozwa na naibu rais William Ruto katika makazi yake rasmi ya Karen. 

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana pia alikuwepo katika mkutano huo ulioongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Gavana wa Embu Martin Wambora. Wengine waliohudhuria ni pamoja na Ndiritu Muriithi (Laikipia), Stanley Kiptis (Baringo), Josphat Nanok (Turkana), Paul Chepkwony (Kericho), Anyang' Nyong'o (Kisumu), Jackson Mandago (Uasin Gishu), Anne Waiguru (Kirinyaga) na Sospeter Ojamoog wa Busia. 

Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakango na Mwenyekiti wa Tume ya Ugawaji Mapato Jane Kiringai pia  walihudhuria. Ruto alikuwa amewaalika Waziri wa Hazina Ukur Yatani, James Macharia (Uchukuzi), George Magoha (Elimu), Peter Munya (Kilimo) na Charles Keter (Ugatuzi). Baraza hilo lilikutana mara ya mwisho mnamo Februari 2021. 

Hiki kilikuwa kikao cha 15 cha kawaida cha baraza hilo ambacho hukutana mara mbili kwa mwaka, na kinaongozwa na DP. Kama mwenyekiti hayupo waziri wa hazina huchukuwa uwenyekiti wa baraza hilo. 

Mwenyekiti ndiye anayeamua ni lini baraza litakutana, na ajenda zake, kwa kushauriana na wanakamati wengine. Wale wanaochaguliwa katika kamati hiyo huhudumu kwa muda wa miaka miwili, na wanaweza kuchaguliwa tena kwa muhula wa ziada. 

Baraza hutoa hilo huleta uiano kati ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti kuhusu hati za bajeti, miongoni mwa masuala mengine ya kiuchumi. 

Baraza hilo linajumuisha Naibu Rais, Mawaziri wa Hazina na Ugatuzi, wawakilishi kutoka Tume ya Huduma za Bunge na Tume ya Utumishi wa Mahakama, mwenyekiti wa Baraza la Gavana, mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Mapato, na wajumbe wa Kamati Tendaji ya Kaunti ya Fedha kutoka kaunti zote.