Jaribio la mwanasheria mkuu kusimamisha kifungo cha jela alichohukumiwa DCI Kinoti lafeli

Ombi la Kihara sasa limepangiwa kusikilizwa Alhamisi.

Muhtasari

•Mwanasheria mkuu katika wasilisho lake anasema kesi ya kukaidi amri ya mahakama iliwasilishwa dhidi ya wahusika wasio sahihi kwani kuzuiwa  kwa silaha za kiraia huwa chini ya bodi ya kutoa leseni za silaha.

Paul Kihara
Paul Kihara
Image: MAKTABA

Jaribio la mwanasheria mkuu wa serikali, Kihara Kariuki kusitisha kifungo cha miezi 4 alichohukumiwa mkuu wa DCI George Kinoti kwa kukaidi agizo la mahakama limeanguka.

Kihara alitaka mahakama isitishe hukumu yake kwa muda ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi la kufuta uamuzi uliotolewa Novemba 18 na Jaji Anthony Mrima.

“Kutokana na aina ya amri zilizoombwa na historia ya kesi hii, mahakama hii ina maoni kwamba amri yoyote itazingatiwa baada ya kusikilizwa kwa maombi hayo,” alisema Jaji Mrima.

Ombi la Kihara sasa limepangiwa kusikilizwa Alhamisi.

Mwanasheria mkuu katika wasilisho lake anasema kesi ya kukaidi amri ya mahakama iliwasilishwa dhidi ya wahusika wasio sahihi kwani kuzuiwa  kwa silaha za kiraia huwa chini ya bodi ya kutoa leseni za silaha.

Kinoti anadai kumwandikia Kihara akimshauri aandikie bodi ya kutoa leseni za bunduki ili kuachilia bunduki za Wanjigis, kulingana na agizo la mahakama.

"Ofisi ya AG pia imewaandikia Jimi Wanjigi na Irene Nzisa kwenda kuchukua bunduki. Hawajafanya hivyo kwa sababu wanazozijua wao wenyewe" Alisema

(Utafsiri: Samuel Maina)