Hakuna mashtaka yoyote dhidi ya Nick Mwendwa:- Faili ya DPP yafungwa

Muhtasari

•Wakili wa Mwendwa, Nelson Havi amesema hatua ya DPP inadhirisha wazi kuwa Mwendwa kukamatwa na kuzuiliwa kwa Mwendwa hakukuwa haki.

Rais wa FKF Nick Mwendwa
Rais wa FKF Nick Mwendwa
Image: FKF

Habari na Susan Muhindi

Idara ya mkurugenzi wa mashtaka ya Umma (DPP)  imefunga faili yakekatika kesi dhidi ya Bosi wa FKF Nick Mwendwa aliyesimamishwa kazi huku wakiendelea na uchunguzi zaidi katika kesi hiyo.

DPP alikuwa amepatiwa siku saba kupendekeza mashtaka dhidi ya Mwendwa lakini amechagua kufunga faili yake.

"Tunataka kufunga faili yetu huku timu yetu ikiendelea na uchunguzi wa kesi hiyo kwa kasi yetu kabla ya kupendekeza mashtaka dhidi yake," alisema DPP.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Milimani Wandia Nyamu aliruhusu ombi la DPP na kuamuru kesi hiyo kufungwa.

Siku ya Alhamisi DPP na DCI walitarajiwa kufahamisha mahakama iwapo walikuwa wamekamilisha uchunguzi dhidi ya Mwendwa na kupendekeza mashtaka yafaayo.

Wakili wa Mwendwa, Nelson Havi amesema hatua ya DPP inadhirisha wazi kuwa Mwendwa kukamatwa na kuzuiliwa kwa Mwendwa hakukuwa haki.

"Nick Mwendwa ameondolewa laamani, hiyo ndio hitimisho yetu. Kufngwa kwa faili kunamaanisha hata uchunguzi umekamilika. Hakuna mashtaka yoyote ya uhalifu dhidi ya Nick Mwendwa" Havi amesema.