Ruto alishirikiana na Gicheru kuhonga mashahidi

Muhtasari

• Ruto na mtangazaji wa radio Joshua Sang walishtakiwa kwa makosa sita ya uhalifu dhidi ya binadamu uliotokana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 nchini Kenya. 

• Kati ya Wasimamizi na Mashahidi wa Mashtaka, wakiwemo Meshack Yebei, Philip Kipkoech, Bett Walter Barasa. Wasimamizi walijumuisha kikundi cha watu mashuhuri waliohusishwa na na/au wafuasi wa Ruto kwa nyakati husika. 

Wakili Paul Gicheru akiwa mbele ya ICC kwa njia ya video kutoka Kituo cha ICC tarehe 6 Novemba 2020 ©ICC-CPI./ICC
Wakili Paul Gicheru akiwa mbele ya ICC kwa njia ya video kutoka Kituo cha ICC tarehe 6 Novemba 2020 ©ICC-CPI./ICC

Naibu mwendesha mashtaka wa ICC James Stewart sasa anasema wakili Paul Gicheru aliwahonga mashahidi akishirikiana na Naibu Rais William Ruto. 

Ruto na mtangazaji wa radio Joshua Sang walishtakiwa kwa makosa sita ya uhalifu dhidi ya binadamu uliotokana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 nchini Kenya. 

Katika waraka wenye kurasa 122 wa tarehe 22 Novemba, Stewart anasema Gicheru anawajibika kibinafsi kwa makosa manane ya kuwashawishi shahidi mmoja mmoja kwa rushwa kama mhusika au kwa pamoja na watu wengine wa mpango wa pamoja kama mshiriki wa moja kwa moja. 

Mpango wa Pamoja ulijumuisha utambulisho, eneo na mawasiliano ya Mashahidi wa Mashtaka, na kutoa na/au kuwalipa faida za kifedha.Au kuwatisha, ili kuwashawishi wajiondoe wakiwa Mashahidi wa Uendeshaji Mashtaka. 

"Lengo kuu la Mpango wa Pamoja lilikuwa kudhoofisha kesi ya muendeshaji Mashtaka katika kesi ya Ruto na Sang kwa kuzuia Mashahidi wa Mashtaka," Stewart alisema. 

Huenda Ruto akashtakiwa kwa kushawishi mashahidi kwa ufisadi chini ya Kifungu cha 70(1)c ambacho kinaweza kumpatia miaka mitano kwa kila kesi.Stewart alieleza kwa kina kwamba Mpango wa Pamoja ulifanyika kufikia Aprili 2013 na kuendelea hadi angalau kukamilika kwa kesi ya muendesha Mashtaka dhidi ya Ruto na Sang mnamo Septemba 10, 2015. 

Ratiba ya matukio muhimu yanayohusiana na utekelezaji wa Mpango wa Pamoja, chati ya uhusiano na muhtasari wa mashahidi viliambatishwa kwenye mawasilisho ya maandishi ya Uendeshaji Mashtaka kuhusu uthibitisho na yamejumuishwa katika Muhtasari huu kwa marejeleo. 

 

Watu hawa ni pamoja na (i). Wasimamizi: Gicheru, Silas Kibet Simatwo na Isaac Maiyo.

(ii). Waunganishi: kati ya Wasimamizi na Mashahidi wa Mashtaka, wakiwemo Meshack Yebei, Philip Kipkoech, Bett Walter Barasa. Wasimamizi walijumuisha kikundi cha watu mashuhuri waliohusishwa na na/au wafuasi wa Ruto kwa nyakati husika. 

Gicheru alifahamisha P-0397 na P-0800 kwamba alikuwa rafiki wa karibu wa Ruto na kwamba walikuwa wamesoma pamoja katika Shule ya Upili ya Kapsabet. 

Uchanganuzi wa simu ya rununu unaonyesha kuwa Ruto alihifadhiwa kama mtu anayewasiliana naye chini ya nambari**. 

Nambari hiyo hapo awali imehusishwa na Ruto na watu kadhaa. Simatwo alikuwa mfanyabiashara mashuhuri nchini Kenya na mshirika wa muda mrefu wa kibiashara wa Ruto. Alikuwa "jicho la Ruto". 

Utekelezaji wa mpango Ili kutekeleza Mpango wa Pamoja, wanachama walitoa michango muhimu kila mmoja. Gicheru na Wasimamizi wengine waliwajibika kwa kazi muhimu za kuongoza na kuratibu shughuli za Wanachama wa Mpango wa Pamoja. 

Waliamua ni Mashahidi gani wa Upande wa Mashtaka walipaswa kulengwa; kujadili na kuamua ni kiasi gani wangepewa na/au kulipwa. 

Pia walihakikisha kwamba fedha zinazohitajika zilipatikana ili kulipa hongo zilizokubaliwa, au angalau sehemu yake na kuwatisha Mashahidi wa upange wa uendeshaji Mashtaka kwa vitisho ikiwa wangekosa kushirikiana.