Vita vyazuka kanisani Kileleshwa kufuatia mzozo wa uongozi, 2 waliojihami kwa bunduki wakamatwa

Muhtasari

•Kikundi kimoja cha waumini 60 kilichoongozwa na mchungaji anayeridhi uongozi Joseph Kanyamu kiliingia katika ofisi za kanisa kwa nguvu baada ya kuvunja mlango wa kioo wakiwa na nia ya kumtimua askofu Joseph Ntombura ambaye inasemekana muhula wake umetamatikana.

Kanisa
Kanisa
Image: BIBLE STUDY TOOLS

Vita vikubwa vilitanda katika kanisa moja iliyo eneo la Kileleshwa baada ya makundi mawili pinzani kutofautiana kuhusu uongozi wa kanisa.

Makasisi na waumini waligeuza kanisa la Lavington Methodist kuwa uwanja wa vita huku wakitupiana ngumi, mateke na maneno makali kufuatia mzozo kuhusu nani angeongoza kanisa ile.

Kulingana na DCI, kikundi kimoja cha waumini 60 kilichoongozwa na mchungaji anayeridhi uongozi Joseph Kanyamu kiliingia katika ofisi za kanisa kwa nguvu baada ya kuvunja mlango wa kioo wakiwa na nia ya kumtimua askofu Joseph Ntombura ambaye inasemekana muhula wake umetamatikana.

Wakati vita vilichacha mlinzi ambaye alishangazwa na waumini waliokuwa wamegeuka kuwa wahuni  alifahamisha polisi kutoka kituo cha Kileleshwa kuhusu kilichokuwa kinaendelea.

Polisi walipofika pale waliweza kuthibiti tukio na kukamata jamaa wawili kutoka kikundi cha mchungaji Kanyamu ambao walikuwa wamejihami kwa bastola aina ya Glock.

Wawili hao, Kisito Matete (43) na Peter Murasi (36)  walitiwa mbaroni baada ya kunyang'anywa batola zao na kupelekwa hadi kituo caa Kilimani.

Polisi wataendelea kulinda na kufuatilia kanisa hilo hadi wakati hali ya wasiwasi kati ya makundi hayo mawili itaisha.