5 wakamatwa kwa kulaghai raia wa Korea mamilioni wakijifanya wauza dhahabu halisi

Walijifanya wangemuuzia dhahabu.

Muhtasari

•Washukiwa walikamatwa kufuatia malalamishi ya Song Sung ambaye hapo awali alikuwa ameonyeshwa vipande vilivyopangwa vizuri na kudanganywa kuwa ni dhahabu.

•Upelelezi ulifichua washukiwa watano waliotambulishwa kama Robinson Gitau 35, Livai Kombo 39, Fatuma Mohammed 28, Eva Kimotho 36 na Utia Kugi 36 ambaye ni raia wa Cameroon.

Washukiwa waliolaghai Mkorea Song Sung
Washukiwa waliolaghai Mkorea Song Sung
Image: TWITTER// DCI

Polisi wanazuilia washukiwa watano wanaodaiwa kulaghai raia wa Korea shilingi milioni 2.9 kwa kujifanya wangemuuzia dhahabu.

Maafisa wa DCI wameripoti kwamba  washukiwa walikamatwa kufuatia malalamishi ya Song Sung ambaye hapo awali alikuwa ameonyeshwa vipande vilivyopangwa vizuri na kudanganywa kuwa ni dhahabu.

Watu wanaoaminika kufanya kazi pamoja na washukiwa walielekeza Bw Sung hadi kwa kampuni iliyojiita Ekweme Enterprises katika mtaa wa Karen ambako alilaghaiwa. Baada ya kupokea pesa za Sung washukiwa waliingia mitini.

Baada ya kukamilisha uchunguzi wa awali wapelelezi walitambua na kukamata washukiwa watano waliotambulishwa kama Robinson Gitau 35, Livai Kombo 39, Fatuma Mohammed 28, Eva Kimotho 36 na Utia Kugi 36 ambaye ni raia wa Cameroon.

Masanduku ya chuma  yenye dhahabu bandia zilizofichwa yalipatikana.

Washukiwa wanazuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani huku raia wa kigeni wanaotazamia kujitosa kwenye biashara ya dhahabu wakiagizwa akuwa makini zaidi kufuatia ongezeko la visa kama kile.