Ruto aandaliwa bonge la sherehe Mombasa!

Muhtasari
  • Wafanyakazi wa hoteli hiyo pamoja na  marafiki wa William Ruto walionekana na keki  huku kwa pamoja wakiimba nyimbo za  kusherekea  siku ya kuzaliwa
DP William Ruto
Image: Twitter

Naibu Rais William Ruto  Jumanne 21, kwenye ziara yake  kaunti ya Mombasa alifanyiwa bonge la sherehe  ya  siku yake ya kuzaliwa.

Ruto ambaye  hakuwa anafahamu kilichokuwa kikiendelea  alishangazwa na nyimbo za siku ya kuzaliwa katika hoteli moja eneo hilo.

Wafanyakazi wa hoteli hiyo pamoja na  marafiki wa William Ruto walionekana na keki  huku kwa pamoja wakiimba nyimbo za  kusherekea  siku hiyo maalum kwake.

Baadhi ya marafiki zake waliokuwepo kufurahia siku hio naye ni  Mbunge wa Nyali Mohammed Ali, Mbunge wa  Malindi Aisha Jumwa,  aliyekuwa Seneta Hassan Omar miongoni mwa wengine. 

Kando na sherehe hio, wakenya mtandaoni ikiwemo familia yake ilimtakia kiongozi  ilimtumia ujumbe wa Kheri ya kuzaliwa

Kupitia twitter, Rachel alimtaja Ruto kama rafiki wa kweli, msiri na baba wa ajabu kwa watoto wao.

 

"Maneno hayawezi kukadiria upendo na usaidizi ambao umeonyesha.Heri ya siku ya kuzaliwa, na Mswada wa Sikukuu njema. Nakutakia baraka nyingi za Mungu na mafanikio makubwa katika kila hitaji la moyo wako," Aliandika Rachel.

Huku akiendelea kuandika ujumbe wa kusherehekea au kuadhimisha miaka 29 katika ndoa, alisema kuwa;

"Siku hii milele inasalia kuwa maalum. Tunaposherehekea siku yako ya kuzaliwa na maadhimisho ya harusi yetu, naweza kusema kwa ujasiri, Ebenezer - Bwana ametuleta hapa. Wewe ni rafiki wa kweli, msiri na baba wa ajabu kwa watoto wetu."