COVID 19: Visa vipya 1, 504 vyaripotiwa; Wagonjwa 401 wapona

Muhtasari

•Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi huku ikiripoti visa vipya 739

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Corona kwa sasa ni 32.4% baada ya visa vipya 1,504 kuripotiwa kutoka kwa sampuli 4,636 ambazo zimepimwa katika kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita.

Idadi hiyo mpya imefikisha jumla ya maambukizi nchini kuwa 285, 654 kutoka kwa sampuli 2, 999, 548 ambazo zimepimwa.

Mtoto wa miezi mitatu na mkongwe wa miaka 95 ni miongoni mwa wagonjwa wapya wa COVID 19. 

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi huku ikiripoti visa vipya 739, Siaya inafuata na visa 97, Nakuru ya tatu na visa 88, Kiambu 69, Uasin Gishu 50 huku kaunti zingine zikiripoti visa chini ya 50.

Wagonjwa 401 wameweza kupata afueni,  103 kati yao ambao walikuwa wamelazwa hospitalini huku 298 wakiponea manyumbani kwao.

Hakuna kifo kilichoripotiwa kutokana na maradhi hayo.

Wagonjwa  752 wamelazwa katika vituo mbalimbali vya afya huku wengine 21, 033 wakiendelea kupokea matibabu nyumbani. Wagonjwa 37 wamelazwa katika ICU.

Chanjo ya Corona

Kufikia sasa jumla ya chanjo 9, 614, 364zimepeanwa. 

Watu 5, 656, 859 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo huku 3, 957, 505 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.