Fisi washambulia na kuua mtu mwingine Kiambu, wakazi washauriwa kuwa waangalifu zaidi

Muhtasari

•Polisi na maafisa wa KWS walitembelea eneo la tukio na kuthibitisha kisa hicho, ambapo fuvu la kichwa, mifupa iliyotawanyika na nguo zilizochanika damu zilipatikana. 

Fuzu la kichwa cha binadamu aliyekuwa amekuliwa na fisi lilipatikana shambani Thika
Fuzu la kichwa cha binadamu aliyekuwa amekuliwa na fisi lilipatikana shambani Thika
Image: MAKTABA

Kisa kingine cha fisi kushambulia mtu katika kaunti ya Kiambu kimeripotiwa.

Kitengo cha upelelezi wa Jinai (DCI) kimesema mkazi mmoja wa eneo la Kang'oki, Thika alifika  katika kituo cha polisi cha Makongeni jioni ya Jumatatu na kupiga ripoti kuhusu  fuvu la kichwa cha binadamu ambacho alipata katika shamba lake la Kandara Investment Scheme.

Polisi na maafisa wa KWS walitembelea eneo la tukio na kuthibitisha kisa hicho, ambapo fuvu la kichwa, mifupa iliyotawanyika na nguo zilizochanika damu zilipatikana. Nyayo za fisi pia zilionekana katika eneo la tukio.

Tukio hili lilitokea masaa machache tu baada ya mwanamume mwingine kushambuliwa na kuuawa katika kisa kama hicho kilichotokea alfajiri ya Jumatatu katika eneo la Witeithie..

DCI wamehimiza wakazi wa maeneo hayo kuwa makini na waangalifu zaidi huku wakiahidi kuwawinda fisi hao wanaohangaisha wakazi na kuwarejesha kwenye mbuga la wanyama.