Waziri Magoha aonya walimu wakuu dhidi ya kufukuza wanafunzi juu ya karo ya shule

CS magoha
CS magoha
Image: Picha:Hisani

Waziri wa Elimu George Magoha, Jumatatu  akikagua ujenzi wa madarasa katika kaunti ya Mombasa aliwaonya walimu wakuu dhidi  ya kufukuza wanafunzi ambao hawajalipa karo.

Magoha  aliwataka walimu wakuu kuwa makini na wanafunzi wakorofi kabla ya mitihani ya KCPE na KCSE, alifichua kuwa wizara tayari imetoa pesa kwa shule kabla ya kufunguliwa kwa kwa  muhula wa tatu  mnamo Januari 4, 2022.

Magoha alisisitiza kwamba hakuna mwalimu ambaye ana haki ya kumnyima mwanafunzi masomo kwa kukosa kulipa karo ya shule 

"Hakuna mtoto Mkenya anayepaswa kuwa nje ya shule kwa sababu ya karo katika mwaka mpya, serikali itahakikisha kwamba pesa zinapatikana kufikia Januari," Waziri alisema 

Alieleza kwamba wamekubaliana na walimu wakuu wakubali kidogo ambacho wazazi watapeleka shuleni kulingana na uwezo wao.

"Kama mzazi hataki mtoto aende shule mwache amweke nyumbani. Maana tumewaambia wakuu kwamba ikiwa ni kesi ya kweli basi wachukue kile ambacho mzazi amemleta shuleni na wakubaliane jinsi ambavyo vingine vitalipwa,”

Magoha alisema watoto ambao wamehusishwa na visa vya kuchoma shule  hawataruhusiwa kurejea humo, na kusema wahusika walio katika kidato cha nne itawalizimu kufanya mitihani wakitoka nyumbani kwao

"Watoto waasi wanaotaka kwenda nyumbani kupumzika, tutawaruhusu. Ikiwa kuna mtoto hataki kwenda shule na anataka kwenda kupumzika na wazazi wake, kufanya mitihani kutoka nyumbani, aende, badala ya kuharibu rasilimali, kwa sababu ni ujinga.kwa sababu anataka  kila mtu ateseke kwa hivyo mnachoma shule na kila mtu anateseka tutakuwa waangalifu sana,” Magoha alisema