Rais Uhuru Kenyatta, Jumatano amemteua Roseline Odhiambo Odede kuwa mwenyeketi wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibidamu ya Kenya(KNCHR)
Odede, ambaye ni Wakili wa Mahakama Kuu, alikuwa jaji na makamu mwenyekiti wa Bodi ya mahikimu kabla ya kuteuliwa kwake
Isitoshe, Rais aliteua wanachama wanne katika KNCHR ambao watakuwa wanafakazi pamoja na Odede.
Walioteuliwa ni ikiwemo na Dennis Wamalwa, Raymond Sang, Sarah Bonaya na Marion Wanjiku ikisubiliwa kuona kama Bunge litaidhinisha majina hayo yaliyopendekezwa na Rais.
Jopo hilo mnamo Oktoba liliapishwa ofisini. Walioliunda ni William Ogara, Regina Mwatha, Jasper Mbiuki, Mary-Anne Njau, Kenneth Ombongi, Akhonya Mutubwa na Habiba Mohammed
Majina yaliyopendekezwa yatatumwa kwa Bunge kujadiliwa na na kama hakutakuwa na dosari kuidhinishwa. Bunge lina siku 28 za kukubali au kukataa mapendekezo hayo ambayo rais ameteua.