Ruto awahimiza wabunge wasipitishe muswada 'tapeli'

Muhtasari

• Ruto alihakikishia wafuasi kuwa mrengo wake una wabunge wengi ambao wanaweza kuzuia muswada huo kupita kama hautafanyiwa marekebisho zaidi.

Naibu rais William Ruto
Naibu rais William Ruto
Image: twitter/DP

Naibu wa rais William Ruto siku ya Jumanne aliwaagiza wabunge wanaoegemea upande wake kuhakikisha muswada wa marekebisho ya vyama vya kisiasa, hutopita iwapo marekebisho hayaturuhusiwa wakati utakuwa ukijadiliwa Bungeni.

Ruto alikuwa akizungumza katika eneo Bunge la Tarbo na kuwahakikishia wakazi kuwa mrengo wake una wabunge wengi ambao wanaweza kuzuia muswada huo kupita kama hautafanyiwa marekebisho zaidi.

"Wasipitishe sheria kwa sababu ya mambo ya kutengeneza ukora, tunataka sheria ambayo inasimamia haki ya kila Mkenya. wale ambao wamezoea kutapeli watu wengine,sasa wamefika mwisho kwa  kuwa hawana mtu wa kutupeli tena "

Muswada huo ambao ulifikishwa bungeni na kiongozi  wa wengi Amos Kimunya, unapendekeza msajili wa vyama kuweza kuwa na nguvu nyingi za kuingilia uteuzi wa vyama na baadhi ya majukumu ya IEBC kuhamishwa kwa msajili wa vyama.

Muswada huo wa mapendezo umepita hatua mbili muhimu imebakia hatua moja tu ambayo wabunge wameandalia vikao maluum Jumatano 29 kujadili.

Naibu Rais alisema walioleta muswada huo wanalazimisha wabunge waupitishe kwa sababu wanajua hawana mambo mengine ya kuonyesha kwa nini wanataka sheria hio ipitishwe wakati huu uchaguzi mkuu unakaribia

"Hawana mtu wa kutapeli ndio sababu saa hizi wanatwambia tusaidieni kwa wabunge tupitishe sheria ndio tusiwatapeli tena" Ruto alisema