COVID-19:Visa vipya 3, 286; Wagonjwa 935 wamelazwa hospitalini

Muhtasari

•Watu 5, 762, 977 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 4, 086, 482 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

Image: HISANI

Wizara ya afya nchini imetangaza visa vipya 3, 286 vya Covid-19.

Kiwango cha maambukizi kwa sasa ni 28.1% huku jumla ya visa vilivyowahi kuripotiwa hapa nchini sasa ikifika  3, 020, 888.

Sampuli 11, 703 ziliweza kupimwa katika kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita. Mtoto wa miezi nane ndiye mgonjwa mpya mdogo zaidi huku mzee zaidi akiwa mkongwe wa miaka 103.

Kaunti ya Nairobi imeripoti visa 1, 176, Nakuru visa 237, Mombasa 187, Kiambu 133, Nyandarua 127, Migori 122, Nyeri 115, Uasin Gishu 114, Siaya 110 huku kaunti zingine zikiripoti visa chini ya 100.

Wagonjwa 260 wameweza kupata afueni, 108 ambao walikuwa wamelazwa hospitalini huku 152 wakipona kutoa manyumbani.

Habari za kusikitisha ni kwamba vifo 4 kutokana na maradhi hayo vimeripotiwa. Jumla ya vifo vya Corona sasa imefika 5,376.

Kwa sasa wagonjwa 935 wamelazwa hospitalini huku wengine 22, 771 wakipokea matibabu kutoka nyumbani. Wagonjwa 39 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Watu 5, 762, 977 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 4, 086, 482 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.